Najaribu kuiva,
Najaribu kuraipeni,
Najaribu kusema viva,
Najaribu kupata mapeni,
Anatomi na zake viva,
Alafu sina eni kichwani
Lakini bado nabukua.
Hivi mumesema kuna kati,
Mimi bado nachana khati,
Hata semesta ipo katikati,
Nikiendelea kucheza kaatii,
Napoteza tu wakati,
Ama niangalie tu skati,
Lakini bado nitabukua.
Ati kuna asainimenti,
Hii haigawanywi ka sakramenti,
Acha nifike pale Imenti,
Angalau nipate vijisenti,
Nilimaanisha yani imenti,
Naendea kale kangu kadenti,
Lakini bado nitabukua.
Ati kuna kazi ya kigrupu,
Hivi ni nani katu grupu,
Nasipendi kazi ya kigrupu,
Kila saa kukutana kigrupu,
Kunawasha kama upupu,
Andika majina yetu ya grupu
Lakini bado nitabukua.
Mbogi tuanzeni kubukua,
Hii egizam inashutua,
Ama bora tutoke tunapumua,
Ama tuanze kuvumbua,
Poplitioli navi ya kifua,
Hii nayo nilichafua,
Lakini nilienda kuifua,
Lakini bado nabukua
©kithi21
K