K

BINTI HUBA

Kaumbika ajabu
Shepu lake la kababu
Mwingi wa adabu
Anipatisha tabu
Binti HUBA!
Asimamapo kibyongo
Kama apinda mgongo
Sijakiona bongo
Kifua chake kidogo
Binti HUBA!
Meno yake kinywani
Weupe wa maziwa asilani
Nyama yake ya ulimi
Hainikifu jamani
Binti HUBA!
Shingo yake ndefu
Ulaini wa mnofu
Nimemvisha mkufu
Wa vito nadhifu
Binti HUBA!
Vazi lake la kitenge
Uafrika kedekede
Tabasamule la umande
Utamuwe peremende
Binti HUBA!
Uso wake angavu
Vidimpo kwa mashavu
Rangiye ndizi mbivu
Chumbani sio mchovu
Binti HUBA!
Nywele zake laini
Mwendo wake makini
Ukimuona hudhani
Kama analake moyoni
Binti HUBA!
Ni nani huyu basi
Moyo wangu augasi
Ajitia mdadisi
Nimwitapo aakisi
Binti HUBA!
©kimjisena