Tarehe kumi na saba, Mwezi qa ukiwa wa tisa,
Kabla ya saba saba, Asubuhi namba tisa,
Habari za msiba, Ishirini kumi tisa,
Kwamba baba yake baba, Kenda kwa nabii Issa.
Ghafla pale nyumbani, Aliweza umwa ndani,
Hakusema kwa nini, Anachoumwa mwilini,
Alipelekwa hodini, Hana nguvu miguuni,
Alikaribishwa ndani, Akapimwa kitandani.
Sindano zile jamani, Hakupata haueni,
Tangu akiwa nyumbani, Kuna kitu mdomoni,
Alitaka wambieni, Hakusema mdomoni,
Akabaki tazameni, Na kulia moyoni.
Mkiwepo mikononi, Akiwaona usoni,
Kujaribu mdomoni, Lililopo mdomoni,
Lakini alishindweni, Na kuwaangalieni,
Akageuka pembeni, Akiwasikitisheni.
Alipokuwa hodini, Siku ya pili hodini,
Kulipatwa na huzuni, Haukuwa duniani,
Tukashtuka vichwani, Machozi toka machoni,
Tukiwaza akilini, Ulitaka sema nini?
Mwaka sasa umepita, Na itazidi kupita,
Nani ataeniita, Kama ulivyo niita?
Nani atakaye ita, Jina lako nikipita?
Nani ataejiita, Jina lako Ulilojiita?
Hebu tujiandaeni, Siku za huko usoni,
Hujui afata nani, Namba mjipangeni,
Huyu kwetu si mgeni, Taarifa mnazoni,
Mabaya yaepukeni, Mengi mazuri fanyeni.
Ndugu zangu pendaneni, Msiweze tenganeni,
Siku hizo pokeeni, Msibadili laini,
Mkibadili laini, Namba mtujuzeni,
Makosa semeaneni, Akikosa mwambieni.
Jasmin Marium, Mohamed na Changala,
Nyie sasa ni walimu, Hakuna tena kulala,
Tupeni zetu elimu, Bila kufanya papala,
Baadae tujikim, Tupate chetu chakula.
Dada zangu Kaundime, Msipeane lawama,
Kaka zangu wa kiume, Msipeane Alama,
Mimi wenu Kaundime, Yangu yote nimesema,
Shairi langu lizime, Niende kwa wangu mama.
©hustoto
H