Nilipata hii kozi,
Toka kwa wangu mzazi,
Haya kuniweka wazi,
Kujifunza ikawa kazi.
Mwanangu nakuusia,
Haya upate sikia ,
Ipo siku tayafaidia,
Moyoni yakiingia.
Nilipokua nasoma,
Kusaidia sikukoma,
Leo naipata heshima,
Matunda kuyachuma.
Nisiyemjua sikuacha,
Mpatia nichopata,
Mwenye njaa mshibisha,
Mgonjwa kumtibisha.
Leo nao wanisaidia,
Maulana analipia,
Dua wazoniombea,
Ni hisani niyowafanyia.
Usije omba rupiya,
Kwa utayowafanyia,
Sije watu tangazia,
Maulana takujibia.
©joseph_s
J