Hunter virus na Corona, Tumekuja kwa maana,
Shetani si muungwana, Afanya yawe mapana,
Msahau maulana, Mpate zake laana,
Wivu mkishikamana, Na mkisaidiana.
Yu anafanya uhuni, Watu wako majumbani,
Ataka wajaribuni, Msiende darasani,
Msiende makazini, Uchumi uwe gizani,
Ili mfeli shuleni, Mkate matumaini.
Elimu ya maanani, Wafata ya duniani,
Ambayo ni ya mbinguni, Mtailudia lini?
Rudini kwenye dini, Hebu hata shtukeni,
Sie twawakumbusheni, Dunia iko meishoni.
Twapita tu njiani, Ili tuwatisheni,
Tokeni huko dhambini, Rudini kwenye imani,
Elimu I hadharani,Ipendeni tu moyoni,
Dawa hio chukueni, Ya swala na Quran.
©hustoto
H