H

KIBERITI

kiberiti kiloshika, Sasa kimeharibika,
Chabaki kuhangaika, Njiti za zidi chomoka,
Umoja ulioshika, Umezidi kuponyoka,
Upendo ulioshika, Umekwisha ondoka.
Njiti jwanza ikitoka, Huenda kuburudika,
Ganda hubadilika, Na kuanza kukwaruzika,
Ganda hukasirika, Na moto waja kuzuka,
Njiti huangaika, Hadi kumumunyuka.
Harufu iki*****a, Njiti wa pili hutoka,
Huja kwa kuruka, Ili Ganda kumshika,
Pale anaposhuka, Moto huja kuwaka,
Njiti hushika, Na majivu hutoka.
Mtu akifika, Hakuna wa kuchomoka,
Hana waliosalimika, Hawawezi kutoloka,
Mtu njiti hushika, Na ganda kutikisika,
Moto ukishika, Wote huharibika.
©hustoto