Umewahi kujaribu, Kuwa Na chako kitabu?
Kikiwa kwa taratibu, Kwa yale yalowasibu?
Chenye mengi majaribu, Chenye kutaka majibu?
Watu wakawa karibu, Kujuwa yaliyosibu?
Walokuwa waarifu, Walipataje adhabu?
Je wale wadanganyifu, Hawakupata aibu?
Wale ni waadilifu, Ni ipi yao swawabu?
Waliokuwa Na bifu, Je walikuwa karibu?
Wasiokuwa na jiko, Waliwapata tabibu?
Wale wenye mi***o, Hawakwenda kwa Zabibu?
Je wale wenye vituko, Waliishiwa sababu?
Wale wenye midundiko, Walikosa taarabu?
Wale wenye maswahibu, Wapata zipi tabu?
Asiefanya wajibu, Alitoa lipi jibu?
Imani yao Kuwa babu, Ilifika kwa katibu?
Wenye ustaarabu, Hawakupata ghadhabu?
Wale ambao ni wakali, Je waliweza kujari?
Wenye zao fahari, Mungu walimtafakari?
Wale wakijivinjari, Haukuwepo ushari?
Wauza medali, Zililudi shekeri?
Hicho ni chako kitabu, Kikiwa na maajabu,
Kikionyesha adabu, Kufanya uwe dhahabu,
Ukipiga hesabu, Wengi utaweza tibu,
Kupata yao majibu, Kujenga waloharibu.
©hustoto
H