Najitimai moyoni,siachi mimi kulia,
Katu sina tumaini,jambo hili lasumbua
Umiza mpaka maini, Ongoya mbona kaanga
Ewe kakangu kwaheri, kwaheri ya kutengana.
Kweli pachangu Ongoya,pamoja tukatambaa
Toka nitoke Ongoya, nilikupenda kanifaa
Mhibu wangu Ongoya,siri zako 'aniambia
Ewe kakangu kwaheri, kwaheri ya kutengana.
Ajali kakufika kaka, chozi mi kadondoa
kichwani kaumia,yangu akili hitatulia
Kapiga teke dunia,ahera kajiendea
Ewe kakangu kwaheri, kwaheri ya kutengana.
Tamwambia nini nyanya,ahadi tuliyompea
Pole baba na mama,kwa mwanya aliotuachia
Sana 'kako kalia, pia wako mpendwa Moraa
Ewe kakangu kwaheri, kwaheri ya kutengana.
Meondoka mapema,hili hatukutarajia
Mungu alaze pema,roho yako ilomfikia
Ulitutendea wema,ni heshima twakupea
Ewe kakangu kwaheri, kwaheri ya kutengana.
©Boldpen.ke
otienoelvis531@gmail.com
©rem-elvis
R