Kuna huyu mwan***e
Ana thamani ya peke
Hunitolea upweke
Haniachi niteseke
Nusura waniteke
Akasimama kidete
Mama!
Mzigo wa kuni kwapani
Ndoo ya maji kichwani
Mimi mdogo mgongoni
Jembe lake begani
Ametokea shambani
Twarejea nyumbani
Mama!
Mchana apike ugali mboga
Usiku awe mke wa baba
Akimkanda kwa mahaba
Amtie moyo kwa huba
Mambo yakimkaba
Japo baba ana vimada
Mama!
Nikikohoa anahaha
Asiweze kulala kwa raha
Ni msukuma au muha
Haijalishi, mimi anijali
Atanipeleka hospitali
Nikamuone dakitari
Mama!
Nikimuudhi hunikosoa
Kwa viboko hunisodoa
Nikilia aanze kunipepea
Akinionya kwa upendo
Ukweli wa haya mambo
Alinidadavulia kitambo
Mama!
Sasa nimekua mtu
Hapo mwanzo sikua kitu
Kamwe sitothubutu
Kusahau wangu utukutu
Mama simpi debe tupu
Namjazia marupurupu
Mama!
©kimjisena
K