Taasubi za kiume, hivi huujenga uume?
Ama huujenga utume, imenibidi niseme.
Wamepiganiwa wa kike, hivi wameujenga uke?
Maskini boichaldi wewe.
Umefanyani mvulana weye,
Mbona usahaulike kiweye,
Ama una mikosi ya Matuko weye,
Maskini kijana wewe.
Mbona hupati tena nafasi,
Umebaki kila mara na wasiwasi,
Utamu umekuwa uchungu kwa nanasi
Maskini barobaro wewe.
Hivi mbona upigwe mawe,
Hivi mbona ukemewe,
Kwani umebadilika kuwa mwewe,
Maskini mvulana wewe.
Mbona wanapendelewa?
Mbona wanaonewa?
Mbona wanakomolewa?
Maskini ghulamu wewe.
©kithi21
K