K

MKULUNGWA

Jasho jingi mwilini
Pesa hana mfukoni
Mabinti awaona ndotoni
Amekosa nini jamani?
Mkulungwa!
Jua lichomozapo
Yeye hula kiapo
Riziki kama ipo ipo
Ikijificha ataipatapo
Mkulungwa!
Atapatapa kila uchao
Kulitafuta tonge walao
Changamoto kibao
Wala hawamtaki kwao
Mkulungwa!
Sarawili anaazima
Na ndala za kichina
Kutwa anaachama
Hana cha kutafuna
Mkulungwa!
Akinywa pombe kali
Mining'inio haikubali
Ila wengine chali
Kwa kahawa ya sukari
Mkulungwa!
Anakazana hachoki
Hata akila blutiki
Mitegoye haikwepeki
Imani ipo siku yatatiki
Mkulungwa!
Nani amhurumie?
Nguo amfulie?
Vyombo amuoshee?
Usiku ampepee?
Mkulungwa!
©kimjisena