H

MWANANCHI

Je wajuwa mwananchi, Ukiwa ndani ya nchi,
Kwenye sikukuu ya nchi, Ipo na ya mwananchi?
Bila wewe mwananchi, Kusingekuwa na nchi?
Kwa kwako mwananchi, Umeipa nini nchi?
Historia ya nchi, Ya jengwa na mwananchi,
Maendeleo ya nchi, Yamtaka mwananchi,
Unavyokuwa mbichi, Leta mema kwenye nchi,
Kwa kwako mwananchi, Umeipa nini nchi?
Sikukuu yako mwananchi, Ya kuishi kwenye nchi,
Ukiketi kwenye kochi, Wengine kwenye benchi,
Wanaume kwenye mechi, Mama kule kwenye pochi,
Kuwa kwenu wananchi, Umeipa nini nchi?
Wewe kama mwananchi, Simama mbele ya nchi,
Ongea kuhusu nchi, Pia wake wananchi,
Faida ya mwananchi, Kwenye hio yake nchi,
Kuwa kwako mwananchi, Umeipa nini nchi?
Kupendwa kwako na nchi, Usije itenda nchi,
Mulikia yako tochi, Giza likitanda nchi,
Imekupa vingi nchi, Tangu uwe mwananchi,
Kuwa kwako mwananchi, Umeipa nini nchi?
Vyombo vya nchi, Vya kufika mwananchi,
Moja ya chombo cha nchi, Gazeti laana Mwananchi,
Lakusaka mwananchi, Uijuze yako nchi,
Kuwa kwako mwananchi, Umeipa nini nchi?
©hustoto