D

OH! LATIFAH

U wa hali gani kipenzi cha watu,
Matamanio ya macho ya mamia ya waume,
Ustadhati uliyewekwa wakfu,
Mzuri mithili ya Bi hadija wa mtume,
Ni raha asali kama imewekwa maziwa,
Na unavyojisitiri kuepusha madhila,
Nafsi yangu inapata mchecheto,
Japo kwa kuishia kukuangalia,
Oh! Latifa moyo wangu umekumbwa na pendo,
Natambua huu ni upendo wangu kwako,
Nipe nafasi maana maneno ni butu pasi vitendo,
Nipe chumba niishi kwenye mtima wako,
Alhamdullilah umeumbwa binti we,
Ni bahati ya mtende kukujua,
Nakupenda kuliko chochote,
Ntakufaa kwa kila hali ije mvua lije jua.
Mr.BLACK NAKUPENDA😘
©delmundothepoet
©delmundo