D

SIKANU YA SHETANI

Leo nimepata ona sikanu ya shetani,
Niiite simu janja kwa lugha ya mtaani,
Ni bahati nimepata haina nywila,
Si ya namba,herufi ama kudetect taswira,
Niliyoyaona mengine yanafurahisha,
Mengine ni kinyaa yanaweza tapisha,
Nlipoiwasha ni mtu yupo Kwa wallpaper,
Ni mtu watu flani humwita shepherd,
Vile mi ni kijana mpenzi wa social medias,
Nkapata curiosity kuread devil's ideas,
profile whatsapp ni baba mchungaji wangu,
camcaption mshkaji wa kweli "damu yangu"
Last status yake kufikiri imenipa tabu,
Nimewaza ama devoo anafanya taarabu!?
"Acha wapige kelele moto wetu sote"
Hii status imenifanya niogope,
kumbe anajua vyenye tunaishi kwa kuigiza,
Tunajimulika tu nuru Katikati ya giza,
nilisikia idd Amini alikufa mwislamu safi,
Ndo mana huku kamsevu "msela mavi",
Hitler na Mussolini ni blood na mnazi,
Amewapa uadmin group la "vijana safi".....
-To be continued-
©delmundo