D

SISI NI KINA NANI?

Wametufanya nyuki wa mashineni,
Tumekubali kuwa simba wa maonyesho,
Tunachezewa Kama chatu wa mazingaombwe,
Tumekuwa kama fisi wamaliziaji.
Tunawasujudu Kama miungu watu,
Huku sisi hatujawahi pendana katu,
Huku wanatuchekea,
Kule tunachekesha,
Tumejisahau lakini hatujachelewa,
Sisi ni kina nani!?
©delmundo