Mungu alikuumba kwa upendeleo,
Na rangi angavu mawio mpaka machweo,
Haiba ya kike na macho ya kusonya,
Ulikuwa mwenye aibu na bidii ya kusoma,
Sasa wewe ni choo cha umma,
Kimbilio la wapita njia,
Bila kujali umri wote wanaingia,
Kwa ofa za chipsi,nyama na bia,
Wanakutumia vile wanavyojisikia,
Unapenda picha kipato hujajaliwa,
Unautumia mwili kwa picha za kudandia,
Honi za magari kwako ni ndoa tosha,
Wakati wako umefika kusema inatosha.
jiulize thamani yako ipo wapi?
©delmundo
D